Elimu ya Ujasiriamali, Kujitambua, na Sera ya Serikali kwa vijana
Wajasiriamali walioamua kujiajiri kupitia kuendesha pikipiki (Bodaboda) Manispaa ya Morogoro wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali, kujitambua na sera ya serikali kwa vijana ili kuwawezesha kudhamini ajira hiyo kwa kuwa inawawezesha kupata kipato cha kutunza familia zao. Pichani ni Afisa maendeleo ya vijana Manispaa ya Morogoro Bi Joycerebecca Paul akieleza ni kwa namna gani serikali inatekeleza sera ya vijana katika kuleta maendeleo. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Asasi ya Care Youth Foundation kwa kushirikiana na Manispaa ya Morogoro ambapo wajasiriamali hao waliamua kujitokeza kupima VVU ili kutambua afya zao.
SHARE