Maadhimisho ya Sikukuu ya Mwl Nyerere 2014
Asasi ya Care Youth foundation kwa kushirikiana na Vission Saccos pamoja na SODA TRUST waliadhimisha sikukuu ya Nyerere day (Mwl Nyerere Commemoration Day 2014) katika vijiji vya Mwalazi na Duthumi wilaya ya Morogoro vijijini. Katika maadhimisho hayo taasisi hizi zimetoa mafunzo ya ujasiriamali, elimu kujitambua na utunzaji wa mazingira kwa wachimbaji wadogowadogo wa madini (Local miners). Kupitia elimu ya ujasriamali, vijana hao waliweza kupata mwamko wa kujihusisha na kilimo cha mbogamboga na matunda ambayo ni njia pekee ya kuwainua wananchi wa vijijini. Picha mbalimbali na video za matukio ya mwl Nyerere zilionyeshwa ikiwa ni moja ya kuwahamasisha wananchi kuendelea kumuenzi Mwl Nyerere kwa kufanya mema na kulinda amani
SHARE