Latest

tes

13 Septemba Yohane Krisostomo
Yohane Krisostomo, kwa Kigiriki χρυσόστομος, khrysóstomos, yaani «Mdomo wa dhahabu» alivyoitwa kutokana na ubora wa mahubiri yake, (Antiokia wa Siria, leo Antakya,nchini Uturuki, 347 hivi - Comana Pontica, Uturuki, 14 Septemba 407) alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli.
Ari yake ilisababisha apendwe na vilevile achukiwe sana. Hatimaye alifukuzwa na Kaisari na kufa uhamishoni.
Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.
Mwaka 1568 Papa Pius V alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Septemba.

Asili na ujana

TAFAKARI YA LEO.

“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Afakari ya kila siku
Jumatano, Septemba 13, 2017.
Juma la 23 la Mwaka wa Kanisa

Kumbukumbu ya Mt. Yohane Chrysostom, Askofu na Mwalimu wa Kanisa

Kol 3: 1-11;
Za 144: 2,3,10-13;
Lk 6: 20-26

BARAKA ZA HERI!

Kila moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa ajili ya furaha. Mungu mwenyewe, katika Utatu Mtakatifu, ndiye Furaha Kuu, ndiye Furaha yote. Masomo yetu ya leo yanatuambia kwamba maskini wapo katika hali salama zaidi kuliko matajiri. Moyo wa Mwanadamu, na uzuri wake na uwezo wake wakupata utakatifu, unachafuliwa, unazimwa na kuharibiwa kwa kuwa mtumwa wa mali na anasa. Tamaa isiyo na mpangilio ya fedha, nyumba, ardhi na vitu vimechafua furaha ya watu wengi na pia furaha ya familia mbali mbali.

Leo Injili inaongelea pia kitu kingine kinachochafua roho nyingi: tamaa ya anasa na kusifiwa (kujenga jina). “Ole wenu ninyi watu wote watakapo wasifu, kwakuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo” (Lk 6: 26). “heri yenu ninyi watu watakapo wachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini na kuruka-ruka, kwakuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii [WA KWELI] vivyo hivyo.” (Lk 6: 22-23).

Yesu anataka kutuambia kwamba watu wakweli wanaomfuata watapata mateso mengi, haitakuwa rahisi njia ya Yesu, mtu anapaswa kusema ukweli hata pale inapo hatarisha maisha yake, kama vile manabii wa ukweli walivyoteseka zamani. Sifa za nabii wa ukweli ni kwamba hakuambii kile ambacho unachotaka kusikia bali anasema ukweli kwasababu ni ukweli. Manabii wengi walipoteza maisha yao kwasababu waliitwa na wafalme ili kutoa unabii juu ya jambo Fulani, lakini wao kwa ujasiri walisema ukweli hata kumrekebisha mfalme na hapo maisha yao yakawa hatarini. Mfalme alitegemea kusikia akisifiwa tu, lakini manabii wa kweli walisema ukweli, huu ndio wito anaotuambia Yesu. Tusiwe kama manabii wa uongo wanaopenda kuongea tu kile ambacho watu wanapenda kusikia bali tuseme ukweli kwasababu ni jambo la kweli.

Sala: Bwana, nisaidie mimi niweze kutafuta Baraka kutoka katika changanmoto na magumu katika maisha. Badala ya kuona misalaba yangu kama uovu, nisaidie mimi niweze kuona mkono wako ukifanya kazi katika kuyabadilisha na hivyo kupata neema nyingi katika vitu vyote. Yesu, nakuamini wewe. Amina

MASOMO NA TAFAKARI YA LEO.

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 13, 2017

MASOMO YA MISA,
JUMATANO,   , SEPTEMBA 13, 2017
JUMA LA 23 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA MT. YOHANE KRISOSTOMI
________

SOMO 1
Kol. 3:1-11

Mkiwa mmefufunuliwa pamoja na Kristo yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu. Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu. Msiambiane uongo, kw akuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate upafamu sawasawa na mfano wake yeye aliuumba. Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi mtumwa wala mwungwana, bali kristo ni yote, na katika yote.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:2-3, 10-13 (K) 9

(K) Bwana ni mwema kwa watu wote.

Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani. (K)

Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako. (K)

Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)
________

SHANGILIO
Zab. 119:28,33

Aleluya, aleluya,
Unitie nguvu sawasawa na neno lako, Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.
________

INJILI
Lk. 6:20 – 26

Yesu aliinua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema,
Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.
Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba.
Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.
Heri ninyi watu watakapowachukia na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni; maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Lakini, ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata.
Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa.
Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia.
Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
________

MTAKATIFU WA LEO.

Tuungane na tusali pamoja.

SALA YA ASUBUHI.

 Kwa jina la Baba.....

Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie.
Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na mwisho nije kwako juu.Amina.

NIA NJEMA.

Kumueshimu Mungu wangu,namtolea roho yangu.
Nifanye kazi nipumzike ,amri zake tu nishike.
Wazo,neno,tendo lote namtolea Mungu pote Roho,Mwili chote changu.
Pendo na uzima wangu.
Mungu wangu nitampenda wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,utakalo hutimia kwa utii navumili.
Teso na matata pia,nipe Bwana neema zako, niongeze sifa yako.Amina.

SALA YA MATOLEO.

Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria,na kwa maungano na sadaka yako kuu.
Ninakutolea sala,matendo,masumbuko na furaha zangu zote za leo.
Ee Yesu ufalme wako utufikie.Amina.

BABA YETU.

Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyo wasamehe na sisi waliyo tukosea.
Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

SALAMU MARIA.

Salamu Maria,umejaa neema Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.

KANUNI YA IMANI.

Nasadiki kwa Mungu,Baba Mwenyezi,muumba  mbingu na dunia.
Na kwa Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,Bwana wetu aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,akazaliwa na  Bikira Maria,akateswa kwa mamlaka ya ponsyo Pilato,akasulibiwa, akafa,akazikwa,akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka katika, akapaa  mbinguni amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi,toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,kanisa takatifu katoliki ushirika wa Watakatifu,maondoleo ya dhambi,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.

AMRI ZA MUNGU.

1.Ndimi Bwana Mungu wako,usiabudu miungu wengine.
2.Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3.Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4.Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5.Usiue.
6.Usizini.
7.Usiibe.
8.Usiseme uwongo.
9.Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10.Usitamani mali ya mtu mwingine.

AMRI ZA KANISA.

1.Hudhuria misa takatifu domonica na sikukuu zilizo amuliwa.
2.Funga siku ya jumatano ya majivu,usile nyama siku ya Ijumaa kuuu.
3.Ungama dhambi zako walau mara moja kwa mwaka.
4.Pokea Ekarist takatifu hasa wakati wa Pasaka
5.Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6.Shika sheria katoliki za ndoa.

SALA YA IMANI.

Mungu wangu,nasadiki maneno yote linayo sadiki na kufundisha kanisa katoliki la Roma kwani ndiwe uliye fumbuliwa hayo,wala hudanganyiki na wala hudanganyi.Amina.

SALA YA MATUMAINI.

Mungu wangu,natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu,neema zako duniani na utukufu mbinguni.Kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi nawe mwamini.Amina.

SALA YA MAPENDO.

Mungu wangu,nakupenda zaidi ya chochote, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza.
Nampenda na jirani yangu kama nafisi yangu kwa ajiri yako.Amina.

SALA YA KUTUBU.

Mungu wangu,nimetubu sana dhambi zangu kwani ndiwe mwema,ndiwe mwenye kupendeza wachukizwa na dhambi.
Basi sitaki kukosa tena nitafanya kitubio,naomba neema yako nipate kurudi.Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI.

Malaika mlinzi wangu,unilinde katika hatari zote za Roho na za Mwili.Amina.

MALAIKA WA BWANA.

K.Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
W.Naye akapata mimba kwa Roho mtakatifu.

Salamu Maria.....

K.Ndimi mtumishi wa Bwana.
W.Nitendewe ulivyo nena.

Salamu Maria.....

K. Neno la Mungu akatwaa Mwili.
W. Akakaa kwetu.

Salamu Maria....

K.  Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W.  Tujaliwe ahadi za Kristu.

Tuombe.

Tunakuomba Ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliyojuwa kwa maelezo ya malaika kwamba, Kristu mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake.
Tufikishwe kwenye  utukufu wa ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.

ATUKUZWE BABA.

Atukuzwe Baba na Mwana na  Roho Mtakatifu,kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina.

K. Moyo Mtakatifu wa Yesu
W.Utuhurumie.

K. Moyo safi wa Bikira Maria.
W. Utuombee.

K. Mtakatifu Yosefu.
W. Utuombee.

K. Watakatifu somo wa majina yetu.
W. Mtuombee.

K.Watakatifu wote wa Mungu.
W.Mtuombee.

Kwa jina la Baba.....✍✍

TUONGEZEE IMANI













Catholic Faith kwa pamoja tulijenge jiji la Mungu.

 We believe that the best way to reach Jesus is through Mary.
 Catholic Faith Admins really we love and trust them.
 Our Feast day is on 15 August every year the Assumption of our dear Mother Mary.
 It was a Final Professional of our dear Brother Patrick who is a member from Catholic Faith group congratulation Brother.
 Rosary is a powerful prayer.
 To Jesus through Mary.
Congratulations to you for your wedding.
 
Copyright ©2017 rrtt • All Rights Reserved.
slid
Design by innocent